IMANI KATIKA MAOMBI.
KWELI SABA ZILIZOMO NDANI YA IMANI:
1Timotheo 3:9; “Wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.”
Mitume na Manabii waliopita, kazi yao kubwa ilikuwa ni kuilinda na kuipigania Imani hii tuliyonayo. Tunaona, walipitia mateso ya kila aina, wapo waliokatwa vichwa, wengine kupigwa na mawe hadi kufa, kutukanwa, kufungwa jela n.k kwa ajili tu ya Imani hii.
2Timotheo 4:7; “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, IMANI NIMEILINDA”
Hata nasi pia tumeagizwa vivyo hivyo, tuishindanie Imani.
Wafilipi 1:27; “Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja MKIISHINDANIA IMANI YA INJILI.”
Je, Imani hii Ina Siri gani? Kwanini wasishambuliwe waislam au wabudha wale wanaoabudu sanamu? Kwanini vita vikubwa vipo kwetu sisi Wakristo?
Twende pamoja tukaangalie Kweli Saba zilizomo ndani ya Imani tuliyonayo ambazo zinamfanya shetani aumize kichwa kwa ajili yetu, yani halali wala hasinzii.
Kweli namba MOJA:
Imani ya Kristo inatupa; UZIMA WA KIMWILI NA KIROHO (WOKOVU).
Wagalatia 5:5; “Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.”
Henoko mtu wa kwanza kutokuonja mauti, alitwaliwa na Mungu kwasababu ya Imani aliyokuwa nayo.
Hata wewe shetani anapokujia na kukushambulia, lengo lake ni kukuzuia au kukufanya ili uiache Imani hii ikupayo uzima wa kimwili na kiroho ili siku moja uje uangamie pamoja nae ktk ziwa la moto.
Ni Yesu pekee ambaye Yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima. Na ili tufike mbinguni ni lazima tufate nyayo zake kupitia Imani aliyotuachia.
Kweli namba MBILI:
Imani ni mlango wa kupitishia – MIBARAKA MBALIMBALI.
Wagalatia 3:9; “Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.”
Yakobo alipokea baraka zake kwa njia ya Imani baada ya kumng’ang’ania yule Malaika ili am-bariki.
Unajua bhana, njia ya kuyafikia Mafanikio huwa haikosi kuwa na kona/ugumu. Huwezi kufikia maono yako kirahisi-rahisi tu.
Mara nyingi shetani hutupiga wakristo kwenye hii sekta ya uchumi, yani unakuta mtu anafanya biashara ila haizai matunda kila anachokifanya hakifanikiwi… Sasa,
wewe ukiona hivyo simama kishujaa, zidi kumng’ang’ania Mungu hadi akubariki, hata kama baraka zako zitacheleweshwa na adui ila kukufikia ni lazima. Usiiache Imani hii kwasababu ya ugumu wa maisha. Sawaa?
Kweli namba TATU:
Imani ni ULINZI TOSHA KTK MAISHA YETU.
1Petro 1:5; “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.”
Shedrack, Meshack na Abednego walilindwa na Mungu wasiangamie ktk ule moto kwasababu ya Imani waliyokuwa nayo. Hata Daniel alitoka salama katikati ya Simba wenye njaa kali kwasababu ya Imani aliyokuwa nayo.
Hata nawe Mkristo unalindwa na Mungu kwasababu ya kiwango cha Imani uliyonayo. Ukiwa na Imani haba, basi usishangae kunigwa na kuchezewa na wachawi usiku kucha. Imani ni kinga na ulinzi tosha, hautaji hirizi wala zindiko. Tunza Imani yako.
Kweli namba NNE:
Imani imebeba – UPONYAJI WAKO.
Luka 18:42; “Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.”
Mtazame yule mwanamke aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, najua kabisa alizunguka sehemu mbalimbali kutafuta suluhu la tatizo lake ila hakufanikiwa. Ila kilichokuja kumponya ni ile Imani aliyoiweka kwa Bwana Yesu kuwa anaenda kumponya, na kweli baada ya kugusa tu pindo la vazi la Yesu, damu ilikata muda huohuo. Kweli namba nne
Imani imebeba – UPONYAJI WAKO.
Luka 18:42; “Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.”
Mtazame yule mwanamke aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, najua kabisa alizunguka sehemu mbalimbali kutafuta suluhu la tatizo lake ila hakufanikiwa. Ila kilichokuja kumponya ni ile Imani aliyoiweka kwa Bwana Yesu kuwa anaenda kumponya, na kweli baada ya kugusa tu pindo la vazi la Yesu, damu ilikata muda huohuo.
Adui anaporuhusiwa kukushambulia na kukuletea udhaifu na masumbufu ya kila aina, lengo lake kuu ni kutaka kukuona ukiiacha Imani ili ukimbilie kwa waganga kutafuta msaada.
Mtazame hata mtumishi wa Mungu, Ayubu; Vita kubwa aliyokuwa nayo ni kwa ajili ya IMANI YAKE THABITI mbele za Mungu.
Nawe usikubali kuiacha Imani hii, kwa ajili ya ugonjwa ulionao, matatizo ya ndoa yako, n.k. Uponyaji unakujia, usikate tamaa, zidi kumwamini Yesu.
Kweli namba TANO:
Imani imebeba – MAJIBU YA MAOMBI YAKO.
Mathayo 21:21-22; “Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.”
Ukuta wa Yeriko ulianguka kwa Imani, Sarah alimpata Isaka kwa njia ya Imani, Gideon na wenzake walishinda Vita kwa njia ya Imani. Hata wewe ndugu yangu utapokea majibu ya maombi yako kwa njia ya IMANI PEKEE.
Kweli namba SITA:
MSAMAHA WA DHAMBI, tunaupata kwa njia ya Imani.
Luka 5:20; “Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.”
Mariamu, dada ake na Lazaro yule aliyefufuliwa na Yesu Kristo, baada ya kujiona ni mwenye dhambi, alienda mbele za Yesu kwa Imani na kujinyenyekeza mbele zake akihitaji asamehewe. Kwasababu ya Imani aliyokuwa nayo, kweli Bwana Yesu alimsamehe.
Hata na wewe, haijalishi uwe umetenda dhambi kubwa kiasi gani, Yesu yupo tayari kukusamehe leo kama vile yule mwana mpotevu alivyosamehewa na Babaye. Usiruhusu hofu ya adui ikuingie na kujiona hustaili tena kupokea msamaha, Noooo, uwe na Imani UTASAMEHEWA TU.
Kweli namba SABA:
Imani – INALETA WATU KWA YESU.
Matendo ya Mitume 16:5; “Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.”
Vile watu wanavyoshuhudia matendo makuu na ya ajabu ambayo Bwana anayatenda na kuyadhihirisha maishani mwetu, kwetu sisi tuliokoka, yanawafanya watu wa mataifa waamini na kufuata Imani yetu.
Ilinde na kuishindania Imani yako mpendwa.
Yuda 1:3; “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU.”
Hizo ndizo kweli Saba zinazomfanya adui atusumbukie Wakristo.
Nina uhakika kabisa, wewe ndugu yangu unayesoma ujumbe huu muda huu haujaokoka kwa bahati mbaya bali kunalo kusudi la wewe kuokolewa kwalo.
Kuna wengine hapa mliamua kuokoka baada ya kuwa mmesumbuka na magonjwa kwa muda mrefu, wengine mliamua kuokoka kutokana na ugumu wa maisha mliopitia, wengine mliokoka baada ya kuvutiwa na kwaya fulani jinsi inavyoimba, wengine mliamua kuokoka ili mpate wachumba, na kadhalika na kadhalika…
Basi sasa, pale tu unapookoka unaianza safari ya imani, na lengo kuu la safari hii ni kuupata Uzima wa Milele. Shida ni kwamba safari hii imejaa milima na mabonde yani kuna kupanda na kushuka, njiani napo pametanda miiba na michongoma kila kona (majaribu na vikwazo)…vyote hivyo vimewekwa na adui ili kutufanya tuiache Imani yetu hii ya THAMANI.
Mungu akubarki Sanaa
Katika jina la Yesu.
Youtube: mwl. Timothy
Facebook: Timothy Sangayoni
Instagram: Timothy Sangayoni
Google: https://lordbreadministry.blogspot.com

No comments