NGUVU YA DAMU YA YESU
Na Mtumishi wa Mungu, Mwl Timothy
DAMU YA YESU INANGUVU YA KUTENDA MAMBO YAFUATAYO;-
Damu ya Yesu inatusafisha na kutuosha dhambi zetu zote, Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, katika vitu ambavyo Mungu amejifunua kwetu katika nyakati hizi za leo ni juu ya ondoleo la dhambi zetu na kuwekwa huru kwa koshwa na kusafishwa. Kusafisha dhambi zetu zote tumepokea kutoka kwa Yesu kristo kupitia Damu yake ya pekee aliyo imwaga pale Msalabani Kalvari, ooh Bwana Yesu asifiwee....
Ukisoma 1Yohana 1;7 neno la Mungu linasema "Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashilikiana sisi kwa sisi na Damu ya Yesu, mwana wake, yatusafisha dhambi yote". Vile vile Ufunuo 1;5 nayo inatueleza kwamba, "Tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake". Kwahiyo unapo tubu tu dhambi zako Mungu anakusafisha na kukuosha kabisa kwa Damu ya Yesu, Hiajalishi umetenda kosa unaloliona kubwa kiasi gani, Damu ya Yesu inauwezo wa kusafisha kabisa.
2. Damu ya Yesu kristo inatutakasa. Kutakaswa maana yeke ni kutengwa kwa ajili ya kusudi maalumu la Bwana, kwahiyo unapo mwamini tu Yesu krito unatakaswa kwa Damu yake, Yaani unatengwa ili kulitumikia kusudi la Mungu la kukuleta hapa duniani. Tunapo lisoma neno la Mnugu linatuambia kwamba, Waebrania 10;19 " Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango ".
3. Damu ya Yesu kristo inatupa uzima. Tunapo yasoma maandiko yanatueleza ya kwamba, Yohana 6;53 "Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. ". Uzima unao ongelewa hapa ni uzima wa Ki Mungu na neno linasema, Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu., kwahyo kinyume chake ni kwamba, Mkiula mwili wake mwana wa adamu na kuinywa Damu yake, mnauzima ndani yenu, ooh Bwana Yesu asifiwe, nguvu pekee ya Yesu kupitia Damu yake mwenyewe ndiyo inayo yupa uzima, Yaani uzima ulionao unapatika katika Damu ya Yesu na si pendinepo, Haleluyah....
4. Damu ya Yesu kristo inatusogeza karibu na Mungu, Kumekuwa na watu mbalimbali wenye kiu ya kumjua na kusogea karibu na Mungu na wamekuewa wakijuliza maswali mbalimbali ya kuwa watawezaje kuwa karibu na Mungu, namimi leo nipo kukupatia ukuweli wa mambo ya kwamba ukitumia Damu ya yesu kristo kwatika Maisha yako nilizima utauona utukufu wa Mungu juu ya maisha yako, cha Muhimu ni kuiita Damu ya Yesu kwa imani yote iliyothabiti ndani yako.
Tukisoma neno la Mungu linatueleza ya kwamba Waefeso 2;13 " Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo." Kuwa mbali maana yake ni kwamba ulikuwa umetengwa na Mungu kwa ajili ya dhambi ulizo mkuwa nazo au zilizo kuwa zikikutumikisha lakini kwa sasa kupitia Damu ya Yesu uwekwa karibu na Mungu. Ooo ni neema ya pekee sana uliyo ipata kupitia Damu ya Msalaba ya Yesu.
5. Damu ya Yesu kristo inatupa uhakika wa kupaingia patakatifu. Waebrania 10;19 " Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu ". Ujasili maana yake ni kwamba hatuna hofu tena ya kuwa karibu na Mungu, wala kutoingia mbinguni kwa sababu ya Damu ya Yesu kristo, kwahiyo Damu ya Yesu ndiyo inayo tufikisha mbinguni, hakuna njia nyingine itakayo kuokoa na jehanamu ya milele isipokuwa Nguvu ya Damu ya Yesu kristo. Na ndiyo maana wale walio waombaji wanaifahamu siri hii ya kwamba pale wanapo jitakasa na kumwomba Mungu huku wakiitumia Damu ya Yesu huwa wanakuwa na ujasili wa kuomba sana kwa Mzigo na kwa ujasili. Na hii ndiyo taofauti yetu sisi pamoja na wale watu wasio mwamini Kristo, napenda kukuambia mpemdwa ya kwamba imo nguvu, nguvu, nguvu ya ajabu sana Damuni mwa Bwana Yesu.
6. Damu ya Yesu inanena mema na kuhimalisha agano. Neno la Mungu linatueleza kuwa, Waebrania 12;24 "na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. ". Danu ya Yesu ndiyo inayo nena mema juu ya shida zako unazo kutana nazo, na muda mwingine shetani na jeshi lake waweza kuwa wamenena mabaya na laana juu yako na ukawa unaishi kwa kuteseka sana, lakini ashukuriwe Mungu kwa ajili ya Damu ya Yesu pale unapo iita huwa inatamka kitu chema juu ya maisha yako na kufuta mabaya yote yaliyo nenwa juu yako. Oooo Bwana Yesu asifiweeee...
7. Damu ya Yesu kristo inatuongezea neema na amani. 1Petro 1;2 " kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu. ".
8. Damu ya Yesu kristo inatulinda na kutushindia wakati wa vita. Unapo kutana na vita yoyote katika maisha yako, tambua ushindi upo pale unapo iita Damu ya Yesu, haijalishi ni vita katika elimu yako, uchumi wako, mahusino yako na hata huduma yako, unapo iita Damu ya Yesu kristo inanena mema na kukushindia na kuangamiza mishale yote ya yule mwovu iliyo kuinukia kupia nyanja zote za maisha yako. Ufunuo 12;11 " Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ".
Yapo mambo mengi sana amabyo ukimwomba Mungu kupitia Damu ya Yesu utaona anakujibu, kitu cha kuzingitia ni kwamba unapo itamka Damu ya Yesu katika maisha yako unatakiwa uwe na imani ya kutosha juu ya hiyo Damu na hapo ndipo nutaona miujiza mikubwa sana katika maisha yako, na hakika na wewe utaungana na miongoni mwa watu watakao yatukuza matendo makuu ya Mungu

Amen amen and Amen sana
ReplyDelete