```*USIMWAMBIE MTU MIMBA YAKO, MUONYESHE MTOTO WAKO!!*
```*USIMWAMBIE MTU MIMBA YAKO, MUONYESHE MTOTO WAKO!!*
Usimwambie mtu NDOTO yako !!! Muonyeshe mafanikio yako
#Mwanzo 37:5-8 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota.Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? WAKAZIDI KUMCHUKIA kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.
Fuatilia 🏃🏃♀uone shida zilizompata baadaye, ndugu zake walipanga kumuua!!
👉chukua jambo hili litakusaidia,Si kila mtu anafaa kumwambia maono yako!!
😷Tunza (maono, ndoto, malengo) yako, kisha yafanyie kazi, yakizaa matunda wambie wote waone vile Mungu amekutendea!!! {MAFANIKIO}.
👉Watu wengi leo wameishia njiani sababu wametoa mambo ambayo bado hayajazaa matunda! na adui akaharibu!.
✍Mfano wa Kwanza ni Yusufu mwenyewe kama ulivyo soma hapo juu
👉Uchumba wa vijana wengi umekufa sababu ya kutangaza hovyo mahusiano yao, hata kabla ya kuchukuwa hatua,
👉Si kila utakae mwambia ndoto zako au malengo yako atafurahi, atakuchekea usoni lakini moyoni anapanga jinsi ya kuharibu!!
✍Una maono ya kufanya biashara flani, si kila mtu anafaa kujua, utajikuta hilo wazo mwenzako kaisha lifanyia kazi, Au anahakikisha hutimizi hayo maono yako!!
Naona ushindi juu yako endapo kama utachukua jambo katika hayo.
*USIMWAMBIE MTU MIMBA YAKO!! SUBIRI UMUONYESHE MTOTO WAKO UTAKAYE MZAA!!*
🙏Mungu awabariki wakati mnatafakari haya.NAWAOMBEA MSIFE KABLA YA WAKATI WENU KATKA JINA LA YESU KRISTO ALIE HAI```

Nimependa mno somo hili barikiwa sana mtumishi WA MUNGU
ReplyDelete