SOMO: NAMNA KIKAO CHA UHARIBIFU KILICHOFANIKIWA KUMCHELEWESHA HAKI YA DANIELI KUPANDISHWA CHEO

 SOMO: NAMNA KIKAO CHA UHARIBIFU KILICHOFANIKIWA KUMCHELEWESHA HAKI YA DANIELI KUPANDISHWA CHEO

Na. Mtumishi mwl.Timothy sangayoni

Danieli 6: 19-28

Shida sio Danieli kupandishwa cheo. Ila je anapandishwa katika majira yapi?

Makubwa 3 katika hoja hii:

1. Wakati Danieli hajui majira ya yeye kupandishwa cheo,  katika ulimwengu wa roho watesi wake walijua na walipanga namna ya kuzuia asipate hicho cheo.

Lazima uombe MUNGU akusaidie kujua majira na nyakati....

Watu wangu wanaangamizwa kwa KUKOSA MAARIFA.  MAOMBI wanayo ila MAARIFA hawana.

Ni lazima uombee akili/maarifa/ufahamu na kuombea macho ya kiroho. Pia inabidi kufunga na kutoa sadaka.

Ni muhimu sana kujua MAJIRA na NYAKATI wakati UNAOMBA. 

1 Mambo ya Nyakati 12: 32

Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao. 

Walipewa akili za kujua wakati na majira. Sio tu kujua majira na nyakati bali na yawapasayo kufanya katika hayo majira na nyakati.  Matumizi mazuri ya muda. Na kila muda lazima ujue una kitu gani cha kufanya.  

Kila muda umebeba yakupasayo kufanya.  Lazima ujue mwakani umebeba nini?  

Danieli alipata ufahamu kwa kusoma vitabu na akapata hayo maarifa na ikampelekea kupata PRAYER POINT ya KUOMBEA.

Ukifanya jambo nje ya majira au majira yakapitiliza na italeta shida sana. Na kuna gharama kutembea nje ya majira.

Majira yakifika MUNGU anakufungulia milango hata kwa kukutafutia watu wa kusaidia.

Mhubiri 3: 1

1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 

Majira ambayo Danieli alikuwa anatakiwa kupandishwa cheo ndo majira ambayo alitupwa kwenye tundu la Simba. 

Watu wengi sana majira ya kupandishwa cheo ndo wanapata majaribu. Wakati wa kuoa/kuolewa/kutafuta kazi/kupanda cheo/kupata mtoto/kuwa na biashara ndo kipindi wanapata majaribu sana.

2. Kwa kuwa watesi wanaufahamu wa majira na nyakati wanalilazimika wakicheza na hayo majira ili yapite bila Danieli kupandishwa cheo.

Watu wengi vitu vyao vimechelewa kwa kutojua majira na Nyakati. 

"Naona Malaika ameshika bango limeandikwa EMERGENCY ISSUE. Omba MUNGU arejeshe Majira na Nyakati hata  kama yameshapita."

Karibu 

Zinarudishwa kwa Jina la Yesu...

 *Have a nice evening*

No comments

Powered by Blogger.