USHINDI UPO JUU YAKO.

 Yesu asifiwe wana wa ufalme wa Mungu,

Naomba leo tujifunze kitu hiki kwa pamoja,

    USHINDI

Nianze kwa kusema sisi ni WASHINDI;- mtu yeyote katika kristo yesu yeye ni mshindi.Tunapigana vita ambavyo mshindi anajulikana tayr, na washindi wenyewe ni mimi na wewe.

     1:KIVIPI SISI NI WASHINDI?🤔

     -kristo yumo ndani ya mwamini ndivyo yanenavyo maandiko.

 1Yohana 4:4

"Ninyi watoto wadogo, mwatokana  na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko  yeye aliye katika dunia".

  2Wakorintho 13:5

" Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe.Au  hamjijui, wenyewe kwamba Yesu kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.

   - oky,,,vitabu tajwa hapo juu vinatuonesha kuwa kristo yu ndani yetu,sasa kama kristo yu ndani yetu na yeye ndiye mwanzilishi wa ushindi basi sisi ni washindi,.

 Kivipi Yesu mwanzilishi wa ushindi?

  -Yohana 16:33

"Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

 - Kristo mwenyewe aliyemo ndani yetu ametuhakikishia kuwa yeye ameushinda ulimwengu ,japokuwa kuwa kuna dhiki ulimwenguni lakini ushindi ameshatupa kristo.

-kama kristo aliushinda ulimwengu na yumo ndani yetu sisi nasi ni washindi.

   2:KAMA SISI NI WASHINDI KWANINI TUNAPITIA CHANGAMOTO?

-Tunapaiatia changamoto katika maisha kwa sababu sisi ni washindi tayar. Shetani hana ushindi wowote ndio maana anatupitisha katika changamoto lengo ni kutufanya tuhisi kwamba hatuna ushindi lakini kiuhalisia ushindi tunao.

  MFANO huu kwauhalisia wa maisha:-

   - mwivi huvamia kwa mtu mwenye nacho na mtu asiyekuwa nacho mwivi hawezi enda pale kuvamia, anafanya hivo kwa mtu ambae anacho tayar  na sio kwa mtu ambae  hana huo ndio ukweli, chukulia mfano huo ili tuelewe kuhusu kwann tunapitia changamoto,.sisi tunaushindi tayr na shetani hana ushindi ndio maana anafanya juu chini kutuletea changamoto katika maisha ili tuhisi kuwa hatuna ushindi, shetani hawezi kuchukua ushindi ulionao kwa sababu aliyemo ndani yako ni mkuu kuliko shetani. Kwahiyo shetani hawezi chukua ushindi ulionao.

1 Yohana4:4

"Ninyi watoto wadogo,mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani

No comments

Powered by Blogger.