SADAKA YA FUNGU LA KUMI.

 1. *MAANA YA FUNGU LA* *KUMI/ZAKA* 

2. *WAZO LA FUNGU LA* *KUMI LILIANZIA WAPI* 

3. *WATOAJI WA* *KWANZA WA FUNGU LA* *KUMI* 

4. *UTOAJI WA FUNGU LA* *KUMI AGANO JIPYA* 

4. *FAIDA ZA KUTOA* *FUNGU LA KUMI* 


Na mwl. Timothy Sangayoni.

🤣🤣🤣 Ety Ujui mshahara unaenda wapi/Boom.

Mtolee Mungu sehemu yake utaona inaenda wapi.

Bila hivo wewe jua kuwa wewe ni mwizi na wezi hawafanikiwi🙆🏻‍♂️🙆🏻‍♂️


 *MAANA YA FUNGU LA* *KUMI:* 


Fungu la kumi ni ¹/10 ya kitu; kama ilivyo ½ tunaita nusu, ¼ tunaita robo n.k. 

Kibiblia, sehemu ya kumi, hasa ya mapato yako ingawa inagusa maeneo mengi mpaka mifugo, mavuno ya mazao n.k, ambayo unaitoa kwa Mungu kama SADAKA inaitwa FUNGU LA KUMI.


Mfano, kipato cha mtu ni 10,000/=, sehemu ya kumi ni 0.1 ya 10000 ambayo ni 1000/=. Hii 1000/= ndio fungu la kumi. Kwenye maandiko, pia neno ZAKA limetumika badala ya fungu la kumi. Haya maneno mawili ZAKA na FUNGU LA KUMI yana maan sawa.


Fungu la kumi ni sadaka ya pekee sana; ni takatifu kwa Bwana.


Neno la Mungu linasema “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, NI YA BWANA; NI TAKATIFU KWA BWANA” (Mambo ya Walawi 27:30). Kwa sababu zaka ni takatifu kwa Bwana, si hiari kutoa; ni lazima uitoe. Tukisoma tena,


Kumbukumbu la Torati 14: 22, iko wazi hapa, kuwa “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka”. Kama Neno la Mungu linatuonya tusiache kutoa zaka, hivi utaanzaje kuila hiyo zaka?. Huwa kuna mazingira yanatokea mtu anajipa sababu tu asitoe zaka anapobanwa na mahitaji yake, anaona aitumie tu hiyo zaka atatoa atakapopata nyingine ILA Neno la Mungu linasema “Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo…” (Kumbukumbu la Torati 12:17).


Kwahiyo, ni lazima, ni muhimu tutoe zaka. Zaka ni takatifu kwa Bwana, tusiile!.


 *WAZO LA FUNGU LA* *KUMI LILIANZIA WAPI:* 


Tuanze kwa kusoma Mwanzo 2:16 – 17 “16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo uta

No comments

Powered by Blogger.