MAVAZI KWA MKRISTO.

 *AGENDA YA MAVAZI KWA MKRISTO*

 

*HAMJAMBO WANA WA MUNGU,NAOMBA NICHANGIE HAPA*

 

KWANZA nakubali kwamba MAVAZI Yana maana kubwa Sana kwa mtu aliyeokoka kwa pande zote mbili,(yaani Kiroho na Kimwili).


Sasa Mara nyingi ukija kwenye hoja hii ya "Mavazi Kwa Mkristo" wapendwa wengi hucharuka na kusaggests kwamba MAVAZI NI SWALA LA KIROHO TU, NA YA KWAMBA ETI HIZI ZA NJE, MUNGU HANA MUDA NAZO, uvae vyovyote,iwe,KAPTULA KIMINI,SKIN JINS, N.K HAIJALISHI, KWA SABABU MUNGU ANAANGALIA ROHO TU.


 *SASA BASI NAOMBA NI WACHALLENGES WAPENDWA WA AINA HII, KWA KUWAPA  MASWALI AMBAYO YANA MAJIBU NDANI, YANAYOHUSINA NA HOJA ZAO* 


 *1* .Kama kweli Mavazi hayana maana kimwili, SWALI!! NI KWANINI "MUNGU" AMBAYE NDIYE "ROHO" HALISI, ANATAJWA KWENYE BIBLIA, KUJALI SANA MAVAZI NA JINSI YA KUVAA HATA YEYE MWENYEWE,"MAANDIKO" YANAONYESHA KWAMBA "MUNGU" ANAVAA MAVAZI YA KUJISITIRI YENYE  STAHA ( *Ufunuo 1:13,YOHANA,ANAONYESHWA MAONO, "KRISTO",AKIWA AMEVAA VAZI REFU LINALOFIKA MPAKA MIGUUNI,KWA MAANA NYINGINE ALIVAA KWA STAHA NA HESHIMA," na Pia ISAYA 6:1",Nabii Isaya anafunuliwa kwenye Maono "Mungu" akiwa amevaa vazi refu linalofunika  mpaka hekalu,SWALI nikwanini huyu "Mungu" ambaye NI "Roho" anajali Mambo ya Mavazi,Wakati sisi tunapuuza na Kusema Jambo la Msingi NI roho na si mwili,JE WEWE NI WA KIROHO ZAIDI KUSHINDA MUNGU AMBAYE ANAVAA KWA STAHA na Heshima,namna hii???*


 **2* Kingine,Kama "Mungu" anaangalia "roho" TU pekee kwa swala la Mavazi,ni kwanini?? 

"Biblia" inatuagiza tutimize. UTAKATIFU WETU, KOTE KOTE,(YAANI KATIKA ROHO NA MWILI, Kwa ujumla,na Si roho peke yake. *( 2 Korinth 7:1)!!!!!*


 *3* Biblia inazungumza kwa HABARI YA MAVAZI YA KIKAHABA *(Mithali 7:10),Je!!! Wewe kwa UELEWA wako unafikiri, Mavazi hayo ni yapi??* 

 *JE Unaweza kupinga kwamba vimini,suruali za mibano,Vikaptula na (blauzi transparent ) ambazo zinaacha wazi Maeneo ya kifuani kwa mwanamke n.k.hazina sifa za kuitwa "Mavazi ya KIKAHABA"????* .


 *4. La nne, ni kwanini Unaposoma Biblia, ukikutana na ANDIKO linalosema makosa yako unaliedit,lakini Lile Linalo KUBARIKI Mambo yako, unaliacha lilivyo.(Mfano, ANDIKO,linalosema Mwanamke asivae Mavazi yampasayo "Mwanaume",na "Mwanamke" Asivae Mavazi ya Mwanamke(Kumbukumbu Torati 22:5),Unapolisoma unatumia hekima na akili nyingi "KUBADILISHA" kwa kujiaminisha kwamba "Mungu" hakuwa na maana hii na hii,ISITOSHE  ili kujifariji zaidi, unatafta mpaka na hekima ya manabii na mitume wa kizazi kipya ambao hawafundishi maadili ya Mavazi kikristo,ili kujilinda,Inapotokea umeonywa kuzingatia mwenendo wa mavazi!!🤔🤔* .


 *5* Najua,Unaweza kuhoji kwamba, *MTUMISHI UNAJUA TUPO KWENYE KIPINDI CHA NEEMA,USITULETEE MAANDIKO YA AGANO LA KALE HAPA,TUPO HURU,* 

SAWA NAMIM

NIKUJIBU HIVI👇👇

 *Biblia Inasema,Je tudumu KUFANYA Dhambi kwasababu neema IPO!!!(Warumi 6:1-2).*

 *Pili swala la kuwa huru unachukuliaje,???* 

Biblia inasemaTumeitwa Kuwa huru kuishi vyovyote TU, Au  kuwa *HURU MBALI NA DHAMBI NA KUWA WATUMWA WA HAKI (Warumi 6:17,22-23)* 


 *Mwisho,Ikiwa Biblia inatufundisha kwamba Mavazi Yanaweza kumtambulisha MTU mpaka tukajua huyu NI Kahaba kutokana na Aina ya Mavazi aliyovaa(Mithal 7:10), Basi Elewa,Mavazi NI kitu cha kujali Sana Kuliko kupuuza,Kwa sababu kupitia Mavazi Yako unasomeka wew NI nani,Usisahua Mavazi NI Kama matendo kiroho,(Isaya 64:6), na Biblia inasema sisi NI Nuru ya Ulimwengu,Kama NI hivyo Ujue "Mungu"mwenyewe,na  mataifa pia ambao hawamjui "Kristo" wanakuangalia kwamba NI kwa vipi unaangaza ulimwengu kwa Nuru ya Mavazi yako🙇🏼‍♀️🙇🏼‍♀️*

No comments

Powered by Blogger.