UWEZO WA MUNGU,JUU YA KUPONYA MAGONJWA, AMBAYO CHANZO, NI URITHI WA ,ADHABU TOKA KWA WALIOKUTANGULIA (LAANA)
KUNA MAGONJWA MENGINE NI ADHABU YA KIROHO INAYOTOKANA NA UASI*
*2 Mambo ya Nyakati 21:13-15*
_“lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; tazama, BWANA atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku.”_
Nataka uone hiyo adhabu ambayo mtu hupewa. Ndani ya adhabu kuna ugonjwa na ameeleza kabisa kuwa huu ugonjwa utaenda kuibukia wapi ni kwenye matumbo yake. Anaposema kwenye matumbo yake, wanaume wana matumbo matatu; wanawake wana matumbo manne:-
➖Kuna tumbo la chakula (chakula hukaa kwa muda mfupi)
➖Kuna utumbo mdogo
➖Kuna utumbo mkubwa
➖Kuna tumbo la uzazi (hili ni kwa wanawake tu)
Kwa hiyo anaposema hayo magonjwa yataenda kwenye matumbo anamaanisha kabisa na yanakuja kama adhabu na ugonjwa huu utakuwa unakuja mara kwa mara
*Kumbukumbu la Torati 28:15-16*
_“Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.”_
Hapa anazungumzia juu ya laana zinazokuja kwa sababu mtu hajafuata maagizo ambayo Mungu amempa kwa wakati ule alipompa. Biblia inasema zitakapomjia na kumpata kutokuwa na furaha, amani, kutokufanikiwa hata kumwama n.k.
Hapo amesema hata kama uko wapi uwe mjini au mashambani usipofuata maelekezo Mungu anayokupa unaweza ukapata baadhi ya vitu nilivyotaja.
*Kumbukumbu la Torati 28:22*
_“BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.”_
Unaweza ukaona hayo magonjwa yote yaliyotajwa hapo kuja kumpata mtu mmoja.
*Kumbukumbu la Torati 28:27-28, 35*
_“BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; BWANA atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.”_
Mpaka hapo nimekuonesha kwa upande wa Mungu, pia zipo kwa upande wa shetani naye ana magonjwa kama hayo na mengine anayofungulia mlango anapogundua kwamba kuna maelekezo umekiuka kufuatana na mapatano yaliyokuwepo na adhabu mojawapo anayoweza kukuletea ni ugonjwa. Sasa si kila ugonjwa chanzo chake ni hiki, ndio maana nilikuwa nakuonesha vyanzo tofauti tofauti.
Dhambi ilipoingia ilituvuruga sana, lakini iliingiza kitu kikubwa mauti (mshahara wa dhambi ni mauti). Sasa toka mauti ilipoanza kutawala, iliachilia vitu vingi sana
Na Mungu akufundishe zaidi
*Imani pasipo maono*
*Imekufa fanyia kazi* *imani*
Yako ebarania 11:6
Mimi ni mwl. Timothy w. Sangayoni
Kwa wenye ya MAGONJWA
Huduma ya Maombi na maombezi yapo.
Mobile: 0769894137
: 0788650274

No comments