UWEZO WA DAMU YA MWANA KONDOO
UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO KATIKA KUONDOA DHAMBI
“Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake” (Zaburi 32:1).
“Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishw mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko KUMBUKUMBU LA DHAMBI KILA MWAKA. Maana HAIWEZEKANI damuya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi”. (Waebrania 10:1-4).
Kuna tofauti kubwa sana kiuwezo juu ya dhambi, kati ya damu ya mafahali na mbuzi ukilinganisha na Damu ya Yesu Kristo.
Biblia inatuambia wazi kabisa kuwa kuna mapungufu yaliyomo katika dhabihu ya damu ya mafahali na mbuzi. Imeandikwa hivi; “Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi” (Waebrania 10:3,4).
Katika dhabihu ya damu ya mafahali na mbuzi kuna; ‘kumbukumbu la dhambi kila mwaka’ kwa kuwa dhabihu hizi HAZIWEZI KUONDOA DHAMBI.
Dhabihu hizi zilipokuwa zinatolewa; dhambi za taifa la Israeli zilikuwa haziondolewi, bali zilikuwa zinasitiriwa au kufunikwa.
Kwa hiyo Kuhani Mkuu wa wakati huo wa Agano la Kale ilimbidi atoe dhabihu hizo kila mwaka ili Mungu aweze kukaa KATI YAO na wala SIYO NDANI YAO!
Kwa maneno mwengine naweza kusema hivi, katika agano la kale Mungu aliwasamehe watu dhambi zao walipotubu LAKINI HAKUZISAHAU BALI ALIZIKUMBUKA!
Ndiyo maana ilibidi kuwekwe agano jipya, kwa kuwa agano la kale lilikuwa na upingufu (Waebrania 8:7)! Kwa sababu hiyo tunasoma ya kuwa Yesu Kristo “amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu y ahadi zilizo bora” (Waebrania 8:6).
Katika agano jipya, Mungu anawasamehe watu wanaotubu dhambi zao, wala hazikumbuki tena! Katika dhabihu ya Yesu Kristo halipo kumbukumbu la dhambi kila mwaka, kwakuwa damu ya Yesu Kristo haifuniki dhambi bali HUIFUTA au KUIONDOA DHAMBI ISIWEPO KABISA! Hebu soma maneno yafuatayo ya biblia; “Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo (Yesu Kristo), alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu;tangu hapo akingojea hata adui wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja AMEWAKAMILISHA HATA MILELE hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye atushuhudia; kwa maana, baada ya kusema, Hili ni agano (Jipya) ni takaloagana nao baada ya siku ziel, anena Bwana, nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika nia zao nitaandika; ndipo anenapo, dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:11 –18)
Oh! Mpendwa msomaji, ni maombi yangu kwa Mungu ya kuwa Roho wake akufunulie zaidi na zaidi juu yauwezo wa damu ya Yesu Kristo. Utaifahamu kweli, nayo hiyo kweli unayoifahamu juu ya damu ya Yesu Kristo itakuweka huru kabisa!
Biblia inatuambi ayakuwa kwa toleo MOJA TU! Haleluya! – ametukamilisha HATA MILELE sisi tunaotakaswa. Pia, kwa toleo moja la dhabihu ya damu ya Yesu Kristo, Mungu hakumbuki TENA KABISA dhambi na uasi tuliotubu. Kwa nini? Kwa sababu Damu ya Yesu Kristo ina uwezo wa kuondoa dhambi zilizo MIOYONI MWETU na zile zilizoandikwa katika VITABU MBINGUNI ili tuhukumiwe.
Hati za Kutushtaki
Mtu anapotubu dhambi zake na kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake; Damu ya Yesu Kristo inafuta dhambi hizo moyoni mwake, pamoja na kufuta dhambi zilizoandikwa katika vitabu vya mbinguni kwa ajili ya kutushitaki.
“Na katika Torati Karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia Mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani Mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa MARA MOJA TU, katika utimilifu wa nyakati amefunuliwa, AZITANGUE DHAMBI KWA DHABIHU YA NAFSI YAKE” (Waebrania 9:22-26)
Je! umewahi kujiuliza kwa nini Yesu Kristo baada ya kufufuka alimkataza Mariamu Magdalena asimguse pale kaburini – Huku baadaye akamruhusu Tomaso aitwaye Pacha amguse?
Je! Yesu Kristo alikuwa hawapendi wanawake? Je! Yesu Kristo alikuwa na kinyongo na Mariamu Magdalena? La hasha – si hivyo! Yesu Kristo alipomkataza Mariamu Magdalena asimguse, alikuwa njiani kwenda kwa Baba – Patakatifu pa Mbinguni, kama Kuhani Mkuu aliyebeba damu yake mwenyewe ili tupate ondoleo la dhambi mbkele ya Mungu na kutupatanisha naye.
Ndiyo maana Yesu Kristo alimwambia Mariamu Magdalena “Usinishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni baba Yenu.., kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu” (Yohana 20:17).
Yesu Kristo aliingia patakatifu kwa ajili yetu kwa damu yake mwenyewe baada ya kupata ushindi mkuu dhidi ya shetani na majeshi yake. Hebu tusome maneno yafuatayo;“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiishakuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na auadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,akaigongomea msalabani isiwepo tena, akaigongome msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” (Wakolosai 2:13-15).
Katika tafsiri ya Kiswahili cha kisasa maneno hayo yanaeleweka vizuri zaidi kwani yanasomeka hivi; “Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu ninyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa ninyi Uzima pamoja na Kristo MUNGU AMETUSAMEHE DHAMBI YA DENI ILIYOKUWA INATUKABILI NA MASHARTI YAKE, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. Huko Kristo ALIWAPOKONYA NGUVU ZAO HAO PEPO WATAWALA NA WAKUU; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwa-buruta kama mateka katika msafara wa ushindi wake” (Wakolosai 2:13-15)
Mungu Baba alipoiona damu ya Kristo imeletwa mbele yake kwa ajili yetu, ALITUSAMEHE DHAMBI TULIZOMFANYIA, AKATUMIA HIYO DAMU KUFUTA DHAMBI HIZO KATIKA VITABU AU HATI ZILIZOANDIKWA ILIKUTUSHITAKI – NA BAADA YAKUZIFUTA DHAMBI HAZIKUMBUKI TENA!
Kama nilivyokuoambia hapo mwanzoni katika agano jipya Mungu anasamehe dhambi na kuzisahau – wala hazikumbuki tena (Isaya 43:25; Waebrania 10:17
Ikiwa umetubu dhambi zako – Mungu amekusamehe na wala hazikumbuki tena kabisa. Kwa kuwa Mungu hazikumbuki dhambi zako tena kabisa, kwa nini wewe unazikumbuka na hata wakati mwingine unamkumbusha Mungu?
Ukizikumbuka dhambi ulizokwishatubu na kusamehewa utajisikia kuhukumiwa rohoni mwako. Na ukijisikia kuhukumiwa moyoni unakosa ujasiri wa kufanya maombi na huduma zingine ulizopewa na Bwana mwisho wake ni kupoa kiroho na kurudi nyuma.
Imeandikwa hivi; “Wapenzi mioyo yetu isipotuhukumu tuna ujasiri kwa Mungu; na lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake” (1Yohana 3:21).
Mimi ni mwl. Timothy w sangayoni.
SOMO LITAENDELEA SIKU YA KESHO.
NA NDIO SIKU YA MWISHO
MUNGU AWABARIKI
SANAAA...

No comments