KUNA UMUHIMU MKUBWA SANAA 

WA KUTUMIA DAMU YA YESU KWENYE MAOMBI

     Tuangalie hapa chini👇👇👇


💻 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 


Ufunuo wa Yohana 12:11


 💫 Damu ya Yesu inanguvu sana ikitumika wakati wa maombi .


💫Damu ya Yesu inanguvu za kumshinda shetani .


💫 Damu ya Yesu inatakasa ( inafuta makosa ) .


💻 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. 


Waebrania 9:22


💫Damu ya Yesu inamnyang'anya shetani umiliki.


💻 9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 


Ufunuo wa Yohana 5:9


10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. 


Ufunuo wa Yohana 5:10


💫 Damu ya Yesu inanguvu za uponyaji .


💫Damu ya Yesu inavunja nguvu za mauti .


 💻 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 


Waebrania 2:14


: 💫Damu ya Yesu inafuta maneno mabaya


: 💫 Itumie damu ya Yesu kuvunja madhabahu ya ukoo inayokuunganisha kwenye ibada za mizimu ,  mashambulizi ya ndoto za wafu na ndoto za nyoka .


💒: 💫Kila kitu kinachokuhusu maishani mwako ambacho shetani amekishikilia au amekificha leo tunakidai , tunamnyang'anya kwa damu ya Yesu .


💒: 💫mpendwa , nikuibie siri kwamba shetani akimiliki malango yako ya kiroho anasumbua sana


.💫 Shetani anatumia wachawi na waganga kufunga maisha ya mtu


💒: 💫 Ardhi iliyofungwa na waganga kupitia matambiko na mazindiko inamadhara sana kiroho


💒: 💫 Achilia damu ya Yesu iondoshe kila mambo ya matambiko na mazindiko yaliyofanyika katika ardhi ya familia , ardhi unayoikalia , na ardhi ya ukoo .


💒: 💫 Peleka damu kwenye kwenye eneo ambalo unafanyia kazi yako au ofisini kwako .


💒: 💫 mpendwa kunaofisi zingine hazikaliki yaani kuna madhabahu ya shetani imesimama kwa lengo la kutafuna wafanya kazi kwa kufukuzwa au kuugua au kufa kabisa .


💫 Kuna kampuni kila meneja akiajiriwa anakimbia kazi , kumbe kuna madhabahu ya shetani imesimamishwa .


💫 Mimina damu ya Yesu iondoshe ile madhabahu .


💒: 💫 Kuna ofisi moja mameneja walikuwa hawadumu lakini kumbe maombi yalipofanyika roho wa Mungu akatuonyesha chini ya kiti kuna kitu kimechimbiwa


💒: 💫 Tuliamkia kuchimba tukatoa hirizi tukaichoma , kuanzia siku hiyo wafanyakazi walikuwa hawasalimiani wakaanza kusalimiana .


.💒: 💫Damu ya Yesu inanena mema .


💒: 💫 Mungu akubariki sana

 N@ mwl. Timothy 

    Email: sangayonitimothy@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.